JINSI YA KUINUA MIZIMU KUTOKA KABURINI.
Habari za wakati huu ndugu msomaji na mfatiliaji wa makala hizi za tiba asili kupitia app hii bora ya tiba asili na jadi. Aghalabu miezi mitatu nyuma tuliekezana namna sahihi ya kuita mizimu kutoka makaburini ikiwa ni sehemu ya kwanza ambapo tulitumia njia rahisi kwa kila mtaalam hata kwa wale ambao si wajuzi wa lugha ya kiarabu.
Leo tungependa tungependa tuelekezane njia ya pili ambayo hii ni mujarabu kwa wale wanaotumia lugha ya kiarabu katika utoaji wa tiba.
Pia unaweza kusoma namna ya kuiita mizimu ije kukutatulia shida zako, chapisho tulilochapisha hivi majuzi.
HATUA ZA KUINUA MIZIMU
Chukua Chumvi Ya Mawe Uisage Iwe Laini, Utaenda Nayo Hadi Katika Kaburi Kisha Utachora Sako (PENTAGRAM) Nje Ya Kaburi na wewe Utakaa Katikati Ya kaburi Kwa Mkao
huu (picha ipo katika kitabu chetu cha uchawi wa zamani) Na Pembeni Kwako Utakua Umeandaa Kivumbasi Kwa Ajili Ya Kumpoza Nguvu Kiumbe Atakae Kuja.
Utavuta Pumzi Mara 21 Na kuiachia Kidogo Kidogo Kisha Utaanza Kusoma ABJEDI, Utaisoma Kwa Mtindo Wa Kuanzia Herufi ya mwisho, Yaani Utaanza na YEE Na Utamaliza Na ALIF.
Utasoma Bila Idadi Hadi Utakapo Ona Makaburi, yanaanza Kuguna Au Katika Kaburi Ulilo Kaa Litaanza Kupumua Kisha Utasema,
"Enyi Mlioko Kuzimu Amukeni Kwa Nguvu za , Hizi Herufi Na Kwa Nguvu Za SUFULI Au Kwa Nguvu Za 0. Wakati Huo Utakua Umechora Pembe Tatu Kwa Kutumia Chumvi Ya Mawe ambayo Itakuwa Kwa Ajili Ya Kuingis Viumbe Au Kiumbe Unae Muita.
Lakini Kumbuka Kabla Ya Kuanza Kusoma
Utalaani ×3 Ili Kujikinga Na Ukorofi Wa Viumbe watakao Kuja, Utassma "AUDHU BILLAHI MINS SHETTWANI RRAJIM × 9.
Na Pia Uwe Umeandaa Vijiti Viwili Ambavyo Utakua Unavifunga Mithiri Ya Msalaba ambao Utaushikilia Wakati Ndo Wanakuja Viumbe.
Njia Hii Ya Kugeuza ABJEDI Pia Unaweza Kuitumia Katika Kufunga Uadui Au Kubatwirisha Uchawi .
Watakapo Kuwa Wanakuja Viumbe Utawaamuru Jinsi Unavyo Taka Na Unaweza kuwaomba Wawe Wasaidizi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA NAMNA YA KUURUDISHA MZIMU ULIOUITA BAADA YA KAZI